Propellerads

Mchezaji huyu wa zamani wa Real Madrid aliyempa mwanae jina la Messi

Aliyekua mchezaji wa kimataifa wa Italia na klabu ya Real Madrid, Antonio Cassano , amefunguka kua  sab anamkubali nyota wa Barcelona Lionel Messi hadi kufikia hatua ya yeye
kumwita mwanae Lionel!!

        
Cassano akiwa na Messi


"Messi ni mchezaji mkubwa katika historia ya soka" aliiambia Italia 1

"Wengi wanasema Maradona alisaidia sana kuchukua kombe la dunia, lakini huo ulikua ni wakati tofauti na sasa"

"Leo ni bora, ndio maana nimempa mwanangu jina lake"

Pia Cassano ameongelea kuwalinganisha Messi na Ronaldo ambapo kadai Messi ni kama Rodger Federer katika soka , wakati Ronaldo ni Rafael Nadal katika soka.

"Yeye na Ronaldo ni wachezaji wakubwa katika soka"

"kama tukifananisha na tenisi Messi ni kama Federer na Ronaldo ni kama Nadal"

Cassano alipata kucheza msimu mmoja pekee Real Madrid akitokea Sampdoria mwaka 2007 , akifunga magoli manne na kutoa usaidizi mara tatu kabla ya kurudi tena klabuni kwake Italia mwaka 2008.
Mchezaji huyu wa zamani wa Real Madrid aliyempa mwanae jina la Messi Mchezaji huyu wa zamani wa Real Madrid aliyempa mwanae jina la Messi Reviewed by Steve on Thursday, May 21, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.