Propellerads

Ronaldo awapa hofu Real Madrid, kisa hiki hapa

                                              
 
Akimaliza msimu wa 2014/2015 bila kombe, Ronaldo anaamini kuna utofauti mkubwa kati ya mafanikio ya ufungaji wa magoli aliyopata Real Madrid na idadi ya makombe aliyoshindaa havilingani. Kiufupi Ronaldo anaumizwa na ukame wa makombe katika klabu ya Real Madrid.
Gazeti la Marca leo limechapisha habari mbaya kwa mashabiki wa Real Madrid , likileta hofu kwamba siku si nyingi Cristiano Ronaldo anaweza kuondoka Los Blancos
Kwa namna Marca walivyoeleza katika stori hiyo, Cristiano Ronaldo anajiona kuwa mtu rahisi Santiago Bernabeu na ana wasiwasi kutokana na muelekea wa sasa wa klabu.
Pia Ronaldo bado ana kinyongo, Marca limesema kwamba mshindi huyo wa Ballon d’Or amechukizwa na Real Madrid kushindwa kumsapoti kuelekea katika sherehe yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 30.
Yote kwa yote, Ronaldo anahitaji ‘Mpango wa Ushindi’ Real Madrid, wakati matajiri wa Ufaransa wanasikilizia kama nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ataonesha nia ya kuondoka Real Madrid.
Tazama ukurasa wa mbele wa gazeti la Maca leo ukija na stori hiyo :

Ronaldo awapa hofu Real Madrid, kisa hiki hapa Ronaldo awapa hofu Real Madrid, kisa hiki hapa Reviewed by Steve on Thursday, May 21, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.