Carlo Anceloti kuondoka Real Madrid, nani anamrithi??!!
Gazeti la kila siku la Hispania, AS, limeikariri Sky Sport
Italia wakiripoti kuwa Carlo Ancelotti anaondoka Real Madrid jumapili ya
juma hili.
Real Madrid watahitimisha msimu wa 2014-15 bila kombe lolote na hali hiyo ya ukame imetia mchanga kibarua cha Ancelotti.
AS wanaripoti kwamba baada ya msimu kuisha, Ancelotti
atakutana na rais wa klabu, Florentino Perez na wawili hao kwa pamoja
wataafikiana kuvubja mkataba unaotakiwa kumalizika juni 30 mwaka 2016.
Wakati Ancelotti akiondoka Bernabeu, tetesi zinasema Real
inamfukuzia Benitez au kocha wa sasa anayeondoka Borussia Dortmund,
Jurgen Klopp.
Benitez, kocha wa zamani wa timu ya vijana ya Real Madrid
ambaye pia aliwapa makombe mawili ya La Liga, Valencia anapewa nafasi
kubwa zaidi ya kumrithi Ancelotti.
Carlo Anceloti kuondoka Real Madrid, nani anamrithi??!!
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 21, 2015
Rating:
