Simba wamtema rasmi Messi wa Tanga.
Messi alisajiliwa na Simba misimu miwili iliyopita, lakini hakupata nafasi ya kutosha kuonyesha cheche zake.
Ingawa alianza kuonyesha cheche wakati wa Abdallah Kibadeni, baada ya Zdravko Logarusic kutwaa ‘madaraka, mambo yalibadilika.
Tokea hapo, Messi huyo wa Tanga aliendelea kupotea taratibu, hadi Simba ilipomtema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema, tayari wamempa ruksa.
“Kweli, Twaha tumemuacha aende. Unajua kama unaona inafikia unalazimika kufanya jambo fulani, basi ni vizuri kulifanya mapema,” alisema.
Hivi karibuni, Twaha amekuwa akisisika akisema kwambaa ana mpango wa kuchana na Simba, hivyo timu yoyote inaweza kumsajili kulingana na maelewano yao.
Simba wamtema rasmi Messi wa Tanga.
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 28, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 28, 2015
Rating:
