Ferguson: Mourinho amebadilika.
Ferguson pia amedai Chelsea iatakua ni timu itakayosumbua sana msimu ujao, babu anadai Mourinho amebadilika sana tofauti na zile alipokua kijana, akienda mbali zaidi na kudai miaka michache ijayo Chelsea itawapa wakati mgumu sana Man Utd.
"Mabingwa siku zote watasumbua" aliongea katika tuzo za chama cha makocha.
"Jose anakijua kikosi chake vizuri, ametulia. Miaka michache ijayo itakua ya mafanikio sana kwa Chelsea.
"Jose amebadilika, anaonekana ana mipango ya muda mrefu na ya wakati huu pia.......miaka michache ijayo itakua migumu kwetu"
Babu huyo wa Man U alidai kua Mourinho alistahili kabisa kuchukua tuzo ya kocha bora wa msimu kwa kua alikua na kikosi bora zaidi.
"Ni mtu mwenye mafanikio. Mshindi"
""Alistahili tuzo, nadhani alikua na kikosi kizuri" alimaliza.
Chelsea msimu huu wakiwa na Mourinho wametumia rekodi ya siku 274 kudumu kileleni mwa ligi, na walichukua ubingwa huku wakiwa na michezo mitatu mkononi.
Ubingwa wa Chelsea msimu huu ulimfikishia Jose Mourinho idadi ya mataji nane tofauti tofauti akiwa na Chelsea ndani ya vipindi viwili tofauti pia.
Ferguson: Mourinho amebadilika.
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 28, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 28, 2015
Rating:
