Sevilla wachukua ubingwa Europa.
HATIMAYE Sevilla wameibuka mabingwa wa ligi ya Europa baada ya kupata ushindi wa magoli
3-2 dhidi ya Dnipro katika mechi ya fainali iliyomalizika usiku wa
jana National Stadium, Warsaw.
Mapema dakika ya 7′ Dnipro waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Nikola Kalinic, lakini dakika ya 28′ Grzegorz Krychowiak akaisawazishia Sevilla.
Dakika ya 31′ Carlos Bacca akaifungia Sevilla goli la pili, lakini Ruslan Rotan akaisawazishia Dnipro dakika ya 44′.
Carlos Bacca ndiye aliyeibuka shujaa baada ya kufunga goli la tatu na la ushindi kwa Sevilla katika dakika ya 73′.
Sevilla wachukua ubingwa Europa.
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 28, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 28, 2015
Rating:

