Ripoti: Bayern wanamhitaji Di Maria.
Mabingwa wa Bundesliga wanamhitaji mchezaji wa Man U Angel Di Maria majira ya
kiangazi.
Wakali hao wa Bavaria wanaungana na Paris Saint Germain katika kuiwinda saini ya Di Maria, lakini wao ndio wanaonekana kupewa nafasi zaidi.
Ripoti kutoka England zinadai Man U wanahitaji kiasi ambacho hakipungui pauni mil. 59.7 kwa ajili ya winga huyo, ambapo Bayern wanweza kutoa dau kubwa zaidi ya PSG ambao wanabanwa na sheria ya matumizi vilabuni.
Di Maria ambaye alikua na wakati mgumu kujiweka katika fomu yake msimu huu, anaweza kupendelea kurudi La liga lakini Real Madrid hawaonekani kutaka kumrudisha tena mu-arjentina huyo.
Di Maria ameonekana katika michezo 33 msimu huu, huku akifunga magoli 4 na kutoa usaidizi zaidi ya mara 12.
Ripoti: Bayern wanamhitaji Di Maria.
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 30, 2015
Rating:
