Mourinho adokeza kua kamwe hakuipenda Real Madrid.
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho amedokeza kua kamwe hakuipenda klabu aliyokua akiifundisha kabla
, Real Madrid.
Mourinho ambaye aliifundisha Madrid kwa miaka mitatu, alirejea tena Chelsea mwaka 2013, na anaonekana kuyafurahia maisha klabuni hapo ambapo msimu huu amewawezesha kuchukua taji la ligi.
Kocha huyo mwenye mbwembwe amedai kua wakati mwingine mtu anajikuta anafundisha klabu asiyoipenda.
"Muda mwingine unafanya kazi na timu usiyoipenda, na wachezaji usiokua na mahusiano mazuri nao" aliiambia Marca.
"Baada ya kua na muda mzuri Chelsea na Inter, nilihitaji kurudi tena katika hali yangu ya kawaida ambayo ni furaha, nimerudi na hapa nia furaha, hali yangu kwa sasa ni nzuri sana. Imara sana"
Meneja huyo wa zamani wa Real Madrid anaamini kua Chelsea wanahitaji kua imara msimu ujao kwani utakua msimu mgumu zaidi kwa klabu.
"Vilabu vyote vikubwa havina furaha, na vitajaribu kupambana" aliongeza.
"Wakati huo huo pia tunatakiwa kufanya vizuri ligi ya mabingwa. Msimu huu tulitoka lakini hatupoteza mechi yoyote lakini tutajitahidi kufanya vizuri katika mpira wa ulaya."
Mourinho adokeza kua kamwe hakuipenda Real Madrid.
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 30, 2015
Rating:
