Tetesi nyingine za usajili Ulaya.
Mdau wangu kama unavyojua wakati huu vilabu vya Ulaya viko kwenye harakati za kuelekea dirisha la usajili, basi leo nakuletea tetesi nyingine za
uhamisho zinazoongelewa sana, tunamuangalia Jackson Martinez, Carlos Bacca, Sami Khedira, Ilkay Gundogan na Edin Dzeko.
Arsenal kumsainisha Jackson Martinez
Mshambuliaji huyu wa Porto anadaiwa kua katika mpango wa kusaini The Gunners. Inadaiwa klabu hiyo iliyoko kaskazini mwa London imemtengea kiasi cha pauni 24.7 na muda tu ndio unaosubiriwa mchezaji huyo kusaini.
Manchester United kumvuta Bacca
Mashetani wekundu wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Sevilla, Carlos Bacca. Mchezaji huyo aliyefunga magoli mawili katika fainali za Europa anaonekana kua na uelekeo mkubwa wa kucheza EPL lakini itawagharimu Man U kiasi kisichopungua pauni mil. 21.3
AS Roma wanamfukuzia Dzeko
Mshambuliaji wa Manchester City ameonekana kuwavutia zaidi waitaliano AS Roma, hata hivyo msimu huu hakua katika kiwango chake, hali inayowarahisishia Roma kumpata kwa urahisi zaidi.
Khedira kuelekea Juventus
Mchezaji anayeonekana kutopewa nafasi sana klabuni Real Madrid anaweza kutimkia Juve.
Kulingana na ripoti, tayari Juve wameshatumiwa ripoti ya afya ya Khedira, na anaonekana yuko fiti. Kinachotakiwa tu kwa sasa ni Juve nao kufanya vipimo vyao.
Man United wamkanusha Gundogan
Manchester United wamekanusha ripoti kua wana mpango wa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan. Hata hivyo mkurugenzi wa Borussia Hans-Joachim Watzke ameshatangaza kumfungulia milango mchezaji huyo, lakini mpaka sasa haijaeleweka ni wapi ataelekea.
Kwingineko Neven Subotic ameongeza mkataba wake na Borussia Dortmund, huku Liverpool wakiwapa mkataba Kolo Toure na Jordon Ibe.
Tetesi nyingine za usajili Ulaya.
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 30, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 30, 2015
Rating:
