Propellerads

Facts kuhusu mechi ya Arsenal vs Aston Villa


                                               



Leo kupitia Dstv channel Super Sport 3 HD, Super Sport 3 na Maximo tutaweza kuangalia mechi kali ya FA Cup final kati ya
Arsenal Vs Aston Villa. Kabla ya mechi nimeona hizi taarifa mtandao mmoja hivi interesting kuzijua kabla hatujaangalia mechi.
Arsenal watakua wanacheza fainali ua 19 na watakua na nafasi ya kuweka rekodi ya kuwa washindi mara nyingi kwa kushinda mara 12. Kwa sasa wana-share record na Manchester united kwa kushinda mara 11.

Arsenal itakuwa ni club ya nne kushinda makombe ya FA mfululizo mara mbili kwa miaka miwili miwili kama wakishinda mechi ya leo. Bolton, Blackburn Rovers,Tottenham Hotspur ziliweza kufanya hivyo.

Arsenal Wenger anatakua manager mwenye mafanikio zaidi kwenye FA Cup kwa kizazi hiki kipya kama akishinda itakua ni mara ya sita ambayo itakua ni moja zaidi ya Sir Alex Ferguson

Aston Villa walishinda FA Cup mara sita kabla ya Arsenal hawajashina kwa mara ya kwanza 1930. Villa wakati inaweka rekodi ya kuchukua FA Cup mara saba, Arsenal ilikua imeshinda mara 3 tu.

Tangu FA Cup ianze mwaka 1871-72, zimetokea fainali mara 5 ambapo timu zote mbili zinaanzia na herufi zinazofanan. Hivi leo tuna Arsenal Vs Aston Villa. Zilizowahi kutokea ni 1881: Old Carthusians vs. Old Etonians; 1902: Sheffield United vs. Southampton; 1953 Blackpool vs. Bolton Wanderers; 1965 Liverpool vs. Leeds United na 2004 Manchester United vs. Millwall.
Facts kuhusu mechi ya Arsenal vs Aston Villa Facts kuhusu mechi ya Arsenal vs Aston Villa Reviewed by Steve on Saturday, May 30, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.