PSG na usajili wa kushtusha kwa Ronaldo
Katika hali ya kutetereka kwa kocha ndani ndani ya Real Madrid , pia klabu kushindwa kuchukua mataji makubwa msimu huu, Paris Saint-Germain wanadaiwa kuleta
mshtuko mwingine klabuni hapo kufuatia wao kuutaka kumnyakua Cristiano Ronaldo.
Imeripotiwa kua PSG wametenga dau la pauni mil. 125 kwa ajili ya kuinasa saini ya nyota huyo kutoka Ureno.
Pia imeripotiwa kua Ronaldo alifanya mazungumzo na raisi wa Real Madrid Florentino Perez kuhusiana na hali klabuni hapo, vile vile matazamio ya klabu msimu ujao.
Hata ivyo Perez ana mambo mengi yanayomngoja wakati huu,huku pia swala la kuamua kocha Ancelloti anaondoka au kubaki likiwa ni miongoni mwa mambo yaliyopo kikaangoni kwa sasa.
Real madrid mkononi wana taji moja pekee la La Liga, pia moja la UEFA na mawili ya Copa del Rey kwa kipindi cha misimu sita ya Ronaldo klabuni hapo, na swala hili limekua miongoni mwa mambo yanayoongelewa sana na mashabiki wengi.
PSG wanayo pesa ya kumvuta Ronaldo, pia ukizingatia mpango wa Platini kurekebisha sera ya matumizi ya pesa kwa vilabu vya ulaya, itawapa nguvu sana.
PSG na usajili wa kushtusha kwa Ronaldo
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating:
