Propellerads

Manchester United kumtumia Giggs kuipata saini ya Bale.

                                 
       

Manchester United wana tumaini la kumpata winga wa Real Madrid Gareth Bale kupitia kocha wao
msaidizi Ryan Giggs.

Giggs ambae pia ni raia wa Wales, ameripotiwa kupewa jukumu la kumshawishi mchezaji huyo aliyeko katika wakati mgumu Los Blancos.

Kwa mujibu wa The Sun, mchezaji huyo ni miongoni mwa shabaha kubwa za kocha Louis Van Gaal na Giggs anatakiwa kufanya juu chini kuhakikisha wanampata katika kipindi kijacho cha usajili.

Bale raia wa Wales anatarajiwa kukipa nguvu zaidi kikosi cha Man U katika safu ya ushambuliaji, hivyo wengi wanachukulia ujio wake utakua kama shujaa.


Manchester United kumtumia Giggs kuipata saini ya Bale. Manchester United kumtumia Giggs kuipata saini ya Bale. Reviewed by Steve on Saturday, May 23, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.