Deco ataja wachezaji wawili ambao alikua hapendi kukutana nao
![]() |
| Deco akipambanana Scholes |
Mchezaji wa zamani wa vilabu vya Chelsea na Barcelona, Deco de Souza ametaja wachezaji ambao walikua wakimpa upinzani mkali mpaka kufikia yeye kutopenda
kupambana nao
Mchezaji huyo mstaafu wa kimataifa kutoka Ureno amewamwagia sifa mkongwe wa Ma U Paul Scholes na pia bosi wa Atletico madrid , Diego Simeone kua ni wachezaji waliokua wakimpa wakati mgumu sana.
"Paul Scholes alikua ni miongoni mwa viungo bora katika historia" Aliiambia Four Four Two.
"Haijawahi kutokea kwa timu kubwa, hajapata kufunga magoli mengi, lakini aliipangilia timu vizuri sana.
"Ninapoangalia mechi,hua nawaangalia sana viungo, wanawarahisishia washambuliaji.
"Scholes na Diego Simeone walikua mwiba kwangu"
Akivichezea vilabu vya FC Porto, Barcelona, Chelsea na Fluminense ya Brazil, kiungo huyo amepata kufunga mabao 39 katika mechi 350 alizocheza, huku akitoa usaidizi mara 66.
Pia ameichezea timu yake ya taifa ya Ureno mechi 75, ni miongoni mwa wachezaji wachache kupata kuchukua kombe la UEFA mara mbili katika vilabu viwili tofaut,i FC Porto na Barcelona.
Deco ataja wachezaji wawili ambao alikua hapendi kukutana nao
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating:
