Propellerads

De Gea kuwafuata Ronaldo, Beckham Real madrid!!

Mlinda mlango wa mashetani wekundu, David De Gea anaweza kufuata uelekeo wa akina Cristiano Ronaldo na
David Beckham Real madrid.



Mchezaji huyo mwenye miaka 4 amekua akihusishwa kwa kiasi kikubwa kutaka kujiunga Los Blancos , hivyo kufuata nyayo za nyota hao wa zamani Man u.

De Gea ambaye ametangazwa mchezaji bora klabuni man U kwa mwaka wa pili mfululizo anaweza kua mchezaji wa sita Man U kushinda uchezaji bora na kisha kutimkia Santiago Bernabou.

David Beckham alitangazwa mchezaji bora Man U mwaka 1997 pia akashinda uchezaji boraEngland mwaka 2003 kabla ya kujiunga Los Blancos majira ya kiangazi mwaka 2003 kwa ada ya pauni mil. 25.

Ruud van Nisterlooy alishinda uchezaji bora klabuni hapo mwaka 2002 na 2003 ambapo baadaye alijiunga Madrid mwaka 2006 kwa ada ya pauni mil. 10.2

Mchezaji mwingine alikua ni Cristiano Ronaldo ambaye kuanzia mwaka 2003, 2007 na 2008 alichukua uchezaji bora Man U ambapo hata hivyo naealijiunga Real Madrid mwaka 2009 kwa ada ya pauni mil. 80.

Gabriel Heinze mwaka 2007 na Javier Hernandez kwa mkopo mwaka 2014 walikua ni miongoni mwa wachezaji waliowahi kuchukua uchezaji bora wa mwaka Man U na kisha kutimkia Los Blancos.
De Gea kuwafuata Ronaldo, Beckham Real madrid!! De Gea kuwafuata Ronaldo, Beckham Real madrid!! Reviewed by Steve on Friday, May 22, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.