Kiungo bora Ulaya ametangazwa
CIES Football Observatory imemtangaza kiungo bora Ulaya msimu huu, ambapo amefikisha point
(alama) 100.
Jopo hilo limemtangaza mchezaji kutoka Chelsea Cesc Fabregas kama kiungo bora ulaya msimu huu huku akiwapiku Paul Pogba, Sergio Busquets na Xabi Alonso.
Alama za wachezaji wote zilikusanywa kwa kuzingatia mambo muhimu katika mchezo kama vile uwezo wa kupanda na kushuka, ukakamavu, kutengeneza nafasi na kupiga mashuti. Uchambuzi ulifanywa kwa viungo wote katika ligi tano kubwa ulaya.
Kiungo kutoka PSG, Marco Verratti ameshika nafasi ya pili akiwa na alama 96.3 , huku Xabi Alonso kutoka Bayern Munich akikamata nafasi ya tatu akivuna alama 91.2.
Katika chati nyingine, Een Hazarameshindwa kutamba mbele ya James Rodriguez kutoka Real Madrid ambaye amekua kiungo mshambuliaji bora ulaya na Thiago Silva ametangazwa kua beki wa kati bora ulaya.
CIES Football Observatory ni jopo la utafiti ndani ya kituo cha kimataifa cha mafunzo ya michezo (CIES) ambapo huchapisha ripoti za kila mwaka kuhusu wachezaji na vilabu ulaya.
Kiungo bora Ulaya ametangazwa
Reviewed by Steve
on
Friday, May 22, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, May 22, 2015
Rating:
