Propellerads

Pique anaweza kustaafu akiwa na miaka 29, kwanini??!!


                                                     


Mlinzi wa zamani wa Manchester United, Gerard Pique amedai kua kama hatakua sawa kuendelea kuichezea Barcelona kwa msimu ujao ni bora akastaafu akiwa na miaka 29 kuliko
kuondoka klabuni hapo.

Mhispania huyo amesema kama hataweza kuchukuliwa tena na msimu ujao, ni bora akastaafu mapema kuliko kuondoka ndani ya klabu hiyo ya Catalan.

"Nitastaafu nikiwa Barca, sijui nitakua na umri gani" aliiambia Marca.

"Nina uhakika na hilo, siwezi kukubali kuvaa jezi ya timu nyingine.

"Kama nikiona mwakani siko vizuri, nitatundika daruga nikiwa na miaka 29.

"Sitaki kucheza klabu nyingine zaidi ya Barcelona."

Pique ni zao la timu ya vijana ya Barcelona, lakini aliondoka kuelekea Manchester United mwaka 2006 kabla ya kurejea tena Barca mwaka 2008.

Mlinzi huyo mwenye 28 kwa sasa, amekua beki wa kutegemewa,ambapo amepata kuchukua La liga mara tano, Copa del Rey mara mbili na klabu bingwa mara mbili pia.

Pique amekua katika kiwango kizuri msimu huu, akicheza mechi 42 na kufunga magoli saba.



Pique anaweza kustaafu akiwa na miaka 29, kwanini??!! Pique anaweza kustaafu akiwa na miaka 29, kwanini??!! Reviewed by Steve on Thursday, May 28, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.