Propellerads

Tetesi: Man U kumtengea pauni mil. 40 nyota huyu wa Real.


Klabu ya Manchester United wanadaiwa kutenga kiasi cha pauni mil. 40 katika harakati za kuifukuzia saini ya nyota wa Real Madrid
, Karim Benzema.



Mashetani hao wekundu ambao wameamua kumuachia moja kwa moja badala ya mkopo mchezaji wao Radamel Falcao, na sasa kocha Louis van Gaal ameelekezea mawazo yake kwa mshambuliaji huyo wa kifaransa.

Kulingana na gazeti la Uingereza, The Sun, Beenzema ni miongoni mwa wachezaji ambao Van gaal anawahitaji sana na yuko tayari kutoa kiasi hicho cha pesa-pauni mil. 40 ili kumpata. Mfaransa huyo pia aliwahi kuwindwa na kocha Sir Alex Ferguson enzi zile kabla ya kusajiliwa Santiago Bernabeu.

Inadaiwa kua Van Gaal ameweka wazi kua anamhitaji mshambuliaji huyo, ukizingatia Van Persie bado hayuko katika kiwango chake, pia Falcao akitimkia Monaco, hivyo ni wazi kua Man U wanahitaji mshambuliaji mwingine.

Haijawa wazi kwa Real madrid kama Benzema ataendelea klabuni hapo msimu ujao, hili litakua wazi kulingana na kocha anaemrithi Ancelloti.


Tetesi: Man U kumtengea pauni mil. 40 nyota huyu wa Real. Tetesi: Man U kumtengea pauni mil. 40 nyota huyu wa Real. Reviewed by Steve on Wednesday, May 27, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.