Ibe, Flanagan kuendelea Liverpool
Jordon Ibe akisaini mkataba mpya na klabu yake ya Liverpool ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka
2020
2020
Winga wa Liverpool Jordon Ibe na beki Jon Flanagan wamesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu yao.
Ibe, ambaye hapo awali alikuwa
akikipiga kwa mkopo katika klabu ya Derby, amedondoka saini ya miaka
mitano ambayo imemuongezea maslahi zaidi kuliko alipokuwa akikipiga
katika ‘academy’ ya klabu hiyo.
Flanagan ambaye amekuwa ametoka
kufanyiwa upasuaji wa pili wa goti, amesaini mkataba wa mwaka mmoja
ambao utamuwezesha kubaki klabuni hapo mpaka mwakani.
Baada ya kusaini mkataba huo mpya Ibe alisema,”Nilifurahi sana
mara baada ya kuitwa kwenye timu hii ya wakubwa, na nimefurahi pia
kupewa nafasi ya kuitumikia klabu yangu. Natumaini nitaendelea kutoa
mchango mkubwa sana kadiri muda unavyokwenda.”
Ibe, Flanagan kuendelea Liverpool
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating:

