Upasuaji ulivyomkwamisha Hazard
Nyota wa Chelsea Eden Hazard
alishindwa kuhudhuria sherehe ambapo alitakiwa kutunukiwa tuzo ya
mchezaji bora msimu kwa waandishi wa habari baada ya kuwa akiuguza
majeraha yake yaliyotokana na upasuaji wa fizi aliofanyiwa hivi
karibuni.
Hazard ambaye alijinyakulia
kura za kutosha kutoka kwa waandishi, huku akipata asilimia 53 na
kumzidi Harry Kane wa Tottenham ambaye alishika nafasi ya pili,
alitakiwa kukabidhiwa zawadi yake katika sherehe zilizofanyika jijini
London.
“Shukrani za dhati ziwafikie Waandishi wa Habari za Michezo nchini Uingereza kwa kunichagua kuwa mchezaji wao wa msimu. Naomba radhi kuwa sitaweza kuhudhuria usiku huu mahala hapo lakini tafadhali mnatakiwa kufahamu kuwa ninajivunia sana juu ya hii zawadi ambayo kwangu mimi ni kubwa sana,” aliandika hivyo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, May 23, 2015
Rating: