Propellerads

Wewe shabiki wa Arsenal ondoa hofu, Wenger ana haya ya kukuambia



Meneja wa Arsenal amesisitiza kua bado kikosi chake kinaweza
kua bora zaidi pamoja na ushindi wao wa kwanza wa Premier League dhidi ya Watford jana jioni.

Gunners wamekua na mwanzo wa kusuasua msimu huu baada ya kuambulia point moja pekee kwenye michezo yao miwili ya mwanzo wakipoteza kwa Liverpool na sare mbele ya Leicester.

Hata hivyo wameshinda mechi ya jana jioni dhidi ya Watford kwa mabao ya Santi Cazorla, Alexis Sanchez na Mesut Ozil ambapo Wenger ana furaha kwa alichokishuhudia.

"Ninaamini mechi ya kwanza tulikua katika pressure kubwa. Tulikua na michezo miwili migumu ya ugenini lakini leo ninaamini tulikua na kiwango kizuri," aliiambia Sky Sports News.

"Ozil hayupo sawa sana, lakini tunataka kutoka kwa Ozili assist nyingi zaidi na magoli na nina imani atafanya hivyo msimu huu, magoli 10 au 15 pamoja na nafasi atakazotengeneza."

Wenger pia amethibitisha kua klabu imekamilisha dili mbili za kuwaleta  Shkodran Mustafi na Lucas Perez.
Wewe shabiki wa Arsenal ondoa hofu, Wenger ana haya ya kukuambia Wewe shabiki wa Arsenal ondoa hofu, Wenger ana haya ya kukuambia Reviewed by Steve on Sunday, August 28, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.