Kamati mpya ya mashindano Yanga iliyoteuliwa na Manji, majina yapo hapa
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ametangaza kamati mpya ya mashindano ambayo imeanza kazi yake
mara moja.
Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedith amethibitisha kuteuliwa kwa wajumbe wa kamati hiyo.
“Mwenyekiti amevunja rasmi kamati ya mashindano iliyokuwa chini ya mjumbe wa kamati ya utendaji iliyopita Mhandisi Isack Chanji mara moja kuanzia leo, Mwenyekiti wa Yanga kwa mamlaka aliyonayo ya kuteua wajumbe watatu wa kamati ya utendaji amemteua Mhandisi Paul Malume kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji mpya na pia kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya mashindano mara moja kuanzia sasa” amethibitisha Deusdetith kaimu Katibu mkuu wa Yanga.
Kamati mpya ya mashindano ambayo Mwenyekiti wake ni Paul Malume inaundwa na wajumbe walioteuliwa ambao ni;
1.Mustafa Ulungo
2.Eng. Mahende Mugaya
3.Abdallah Bin Kleb
4.Jackson Maagi
5.Samwel Lukumay
6.Hussein Nyika
7.Athumani Kihamia (kutoka Arusha)
8.Felix Felician Minde (kutoka Mwanza)
9.Leonard Chinganga Bugomola (kutoka Geita)
10.Omary Chuma
11.Hussein Ndama
12.Hamad Ali Islam
13.Yusuphed Mhaden
14.Beda Tindwa
15.Moses Katabalo
16.Roger Lamlembe
Kwa maana hiyo, Mhandisi Isack Chanji atabaki kuwa mshauri kamati hiyo mpya ya mashindano.
Kamati mpya ya mashindano Yanga iliyoteuliwa na Manji, majina yapo hapa
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 28, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 28, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment