Unawaza kuhusu Rashford!!, Mourinho amzungumzia zaidi
Meneja wa Manchester United amesisitiza kua Marcus Rashford atapata
nafasi nyingi zaidi kucheza kikosi cha kwanza msimu huu.
Tangu ujio wa nyota wapya kama Zlatan Ibrahimovic, Rashford amekua akikaa benchi lakini jana amekua mkombozi baada ya kuingia na kuipatia United bao pekee na la ushindi dhidi ya Hull City.
"Yuko vizuri. Najua yuko vizuri sana tangu msimu uliopita, lakini niko nae kila siku naona yupo vilevile. Mechi mbili tulihitaji ushindi dhidi ya Leicester na leo usiku. Ameingia na ametupa ushindi adimu," Mourinho aliwaambia waandishi.
Mourinho azungumzia ushindi finyu dhidi ya Hull City
"Yuko tofauti kuliko (Wayne) Rooney, yuko tofauti kuliko Zlatan, kwa hiyo kila mtu anamfurahia na tuna furaha na kikosi. Nina wiki mbili kaba ya mechi ijayo. Ninahitaji kuwachambua wapinzani na kuangalia jinsi vijana wangu watakavyorejea kutoka michezo ya kimataifa.
"Anaweza kucheza lakini anaweza kua benchi. Sijajua. Ninatakiwa kuchambua. Kitu muhimu ni kwamba anajitahidi sana. Tunaanza mechi akiwa nyuma ya Zlatan, lakini tunaweza kuanza mechi akaanza badala ya Zlatan, kwa hiyo kijana anaenda kuanza mechi nyingi ki ukweli."
Unawaza kuhusu Rashford!!, Mourinho amzungumzia zaidi
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 28, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 28, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment