Propellerads

Simba walivyokamatika kwa JKT Ruvu




Baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ndanda FC, Simba SC
imejikuta ikibanwa na maafande wa JKT Ruvu na kulazimishwa suluhu (0-0) katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliomalizika kwenye uwanja wa taifa.

Simba ilipambana kutafuta goli dakika zote za mchezo lakini mambo yalikua magumu kwao kutokana na kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na golikipa wa JKT Ruvu Said Kipao.

Licha ya kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Fedrick Blagnon na Jamal Mnyate na kuwaingiza Mwinyi Kazimoto na Ibrahim Ajib lakini bado hawakuweza kubadili matokeo.

Ikumbukwe May 21 2016, JKT Ruvu waliikomalia Simba na kuitandika bao 2-1 kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu msimu uliopita.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 4 baada ya mechi mbili wakati JKT Ruvu wao wamefanikiwa kupata pointi 1 kwenye mchezo wao wa ufunguzi VPL msimu huu.
Simba walivyokamatika kwa JKT Ruvu Simba walivyokamatika kwa JKT Ruvu Reviewed by Steve on Saturday, August 27, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.