Unadhani Mata na Mourinho haziivii!!, haya ni makubaliano waliyoyafanya
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekua na hali flani
hivi ya kutoelewana na Juan Mata, lakini sasa inaelezwa wamefikia makubaliano fulani ndani ya Od Trafford.
Mhispania huyo amekua akianza kwenye mechi zote zilizopita za United msimu huu na kuwashangaza wengi kutokana na kuwahi kutokuelewana na Mourinho siku za nyuma.
Alipokua Chelsea, kocha huyo Mreno hakumpanga kiungo huyo mshambuliaji kama chaguo lake la kwanza na mwisho akamuuza kwa Red Devils mwezi januari 2014 pamoja na kua mchezaji bora wa mwaka klabuni mra mbili mfululizo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Daily Telegraph, Mourinho na Mata wamefikia makubaliano fulani United, ambapo Mata anaelewa wazi kua hatokua miongoni mwa wachezaji chaguo la kwanza msimu huu.
Ripoti pia zinazidi kudai Mourinho atampendelea zaidi mchezaji mpya, Henrikh Mkhitaryan katika wingi ya kushoto katika wiki zijazo hivyo Mata atajikuta akiishia benchi.
Inaaminika kua mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea ataendelea kuwepo Man United mpaka dirisha la usajili lijalo.
Unadhani Mata na Mourinho haziivii!!, haya ni makubaliano waliyoyafanya
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 27, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 27, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment