Schwensteiger afunguka uhusiano wake na Mourinho uko vipi
Bastian Schwensteiger ambaye hivi karibuni ametoswa katika
kikosi cha kocha Jose Mourinho klabuni Manchester United sasa amefunguka jinsi uhusiano wake ulivyo na Mreno.
Nyota huyo alizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wake wa mwisho timu ya taifa ya Ujerumani dhidi ya Finland kesho Jumatano, akisistiza kwamba ana mahusiano mazuri tu na kocha bosi huyo wa United pamoja na kulazimishwa kufanya mazoezi na kikosi cha akiba.
Wakala wa Joe Hart athibitisha kuelekea klabu hii ya Serie A
"Matakwa yangu yalikua ni kuendelea kuichezea Manchester United. Sina matatizo binafsi na Mourinho."alifunguka.
"Ninajua nini klabu na Mourinho wanataka, na mimi mwenyewe najua nini ninataka. Ni uhusiano wa heshima kati yangu na kocha, mimi, na klabu, hiyo ni muhimu sana kwangu.
"Kitu kimoja cha uhakika, siachi kucheza mpira. Bado naamini katika uwezo wangu. Bado ninaweza kuisaidia Manchester United kama nikipewa nafasi.
"Ndoto yangu haswa ilikua ni kuendelea kuichezea Manchester na kuisaidia"
Pia aligusia uvumi wa kutaka kuhamia MLS kwa baadae endapo akiondoka Man United.
"Dirisha la usajili MLS limeshafungwa. Kwa hiyo msimu huu haitatokea." alimaliza.
Schwensteiger afunguka uhusiano wake na Mourinho uko vipi
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment