Rooney aweka wazi wakati atakaostaafu kimataifa
Kapteni wa England, Wayne Rooney ameweka wazi kua ataachana
na soka la kimataifa mara baada ya fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United ndiye mfungaji bora zaidi wa timu ya taifa ya England katika historia ambapo anaamini kombe la dunia miaka miwili ijayo utakua wakati sahihi wa yeye kuachana na timu ya taifa.
"Tukielekea urusi, nadhani ndio utakua wakati wangu sahihi wa kusema kwa heri kwa mpira wa kimataifa. Ni wazi kwamba hili ni juu ya Sam (Allardyce), lakini ndipo utakua mwisho wangu na England, itakua baada ya kupanda na kushuka lakini nitakua najivunia," aliwaambia waandishi.
"Nilianza kucheza mpira wa kimataifa nikiwa na miaka 17, kwa hiyo nikifikisha 32 miaka miwili ijayo nitakua nimecheza kwa miaka 15 kwa hiyo nafikiri ni muda sahihi wa kumaliza."
Rooney aweka wazi wakati atakaostaafu kimataifa
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment