Baada ya mambo kuwa mabaya Man City, huku ndipo anakoelekea Joe Hart
Mlinda mlango wa England, Joe Hart hayumo katika mipango ya kocha
Pep Guardiola kwa Manchester City msimu huu, na sasa wakala wake ameweka wazi klabu atakayoelekea.
City wakiwa wamemsajili aliyekua golikipa wa Barcelona, Claudio Bravo wiki iliyopita, hatma ya Hart klabuni hapo ilikua haieleweki.
Ilikua tetesi zikienea kwamba mlinda mlango huyo alikua amefunguliwa mlango wa kutokea City, sasa wakala wake, Jonathan Barnett amethibitisha kwamba atajiunga na klabu inayocheza Serie A ya Torino kwa mkopo.
"Ni kweli, Joe Hart ataichezea Torino," Barnett aliiambia Tuttosport.
"Imekamilika. Golikipa ameikubalia klabu na Manchester City wamemwashia taa ya kijani."
Baada ya mambo kuwa mabaya Man City, huku ndipo anakoelekea Joe Hart
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment