Kina Tegete waifikisha Yanga mahakamani, mkasa kamili upo hapa
Klabu ya soka ya Yanga, imeonekana ina kesi ya kujibu kuhusiana na
madai ya wachezaji Jerry Tegete, Omega Seme na Hamis Thabit.
Wachezaji hao wameonekana kuwa wana haki ya kulipwa fedha zao za usajili na klabu hiyo.
Makamu Mwenyekiti Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Raymond Wawa, amesema Yanga ina kesi ya kujibu.
Kwa mujibu wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa jana, Yanga imeonekana ina kesi ya kujibu lakini kesi zake zote zimesogezwa wiki ijayo.
Sputanza ndiyo ilifungua kesi hiyo ikiwawakilisha wachezaji hao akiwemo Tegete ambaye alikuwa mchezaji nyota na tegemeo la ufungaji kwa Yanga.
Kina Tegete waifikisha Yanga mahakamani, mkasa kamili upo hapa
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment