Mourinho awapongeza mashabiki wa Chelsea kwa maneno haya

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho amewasifia mashabiki wa klabu hiyo
kwa walichokionesha kwenye mechi waliyoshinda kwa 2-1 dhidi ya Dynamo Kiev.
Free kick ya Willian katika dakika za mwishoni iliwapa point tatu muhimu wakali hao wa London wakiwa Stamford Bridge ambapo wamewapiku Dynamo na kushika nafasi ya pili katika kundi G.
Wiki hii iliripotiwa kua Mourinho ambaye nafasi yake kwa sasa ipo katika msukumo mkubwa baada ya kupoteza kwa 3-1 mbele ya Liverpool, hatafukuzwa na mmiliki wa klabu Roman Abramovich baada ya mashabiki kuendelea kumuunga mkono kocha huyo Mreno.

Mourinho ametoa pongezi zake kwa mashabiki jana baada ya ushindi, akikazia kua ni ngumu mtu kuendelea kua shabiki wa Chelsea katika kipindi hiki kigumu.
"Kipindi niliporudi klabuni, jinsi uwanja ulivyonikaribisha ilishangaza, lakini huwezi kulinganisha na leo," aliwaambia waandishi kwenye mkutano baada ya mechi.
"Leo ni siku ambayo matokeo sio mazuri. Mnaomba mwongozo wangu. Mashabiki wanaona vitu kwenye vyombo vya habari lakini ni ngumu kuamini wanavyosema leo. Wanasema 'ngoja afanye kazi' . Wachezaji wameonesha tena wanataka kushinda.
"Ni virahisi watoto kwenda shule na jezi ya Chelsea kama tukiwa tunashinda. Inawezekana walikua wanazomewa na wenzao wiki kadhaa zilizopita."
Chelsea watasafiri hadi Britania Stadium kupambana na Stoke City ambao waliwachapa Blues kwa matuta kwenye michuano ya League Cup jumamosi jioni.
Mourinho awapongeza mashabiki wa Chelsea kwa maneno haya
Reviewed by Steve
on
Thursday, November 05, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment