Arsene Wenger amelaumu 'kiwango kibovu' baada ya kipigo cha Bayern Munich

Arsene Wenger amesema Arsenal walijidhoofisha wenyewe
kwa 'kiwango kibovu sana' kujilinda jana usiku kufuatia kupoteza kwa 5-1 dhidi ya Bayern Munich jana usiku.
Hali tete kwa Gunners ndani ya Allianz Arena ilianza kipindi cha kwanza tu pale magoli ya Robert Lewandowski, Thomas Muller na David Alaba yaliwafanya Bayern Munich kuongoza kwa 3-0 ndani ya dakika 45.

Arjen Robben na Thomas Muller walimaliza karamu ya magoli, hakuna aliyeongeza bao jingine kwa Arsenal mbali ya lile pekee la Olivier Giroud ambapo ilishuhudiwa Arsenal wakizamishwa kabisa baada ya kupata ushindi wa 2-0 nyumbani kwenye mechi ya kwanza.
"Unatakiwa uwape sifa kwanza Bayrn Munich kwa kiwango chao na ukiongezea hapo tuliwarahisishia sana," Mfaransa huyo aliiambia tovuti rasmi ya klabu ya Arsenal.
"Ilikua ni perfomance mbovu ya ulinzi na tulikua na kiwango kibovu sana kwenye ulinzi. Hatukua katika mbio, cha kushangaza ni kua tulipoenda mbele tulitengeneza nafasi nzuri.
"Tulikua na nafasi nzuri ya kufunga mapema lakini kwa kiwango cha ulinzi kama vile, huendi popote."
Arsenal wako nafasi ya tatu kundi F, point sita nyuma ya vinara Olympiacos na Bayern Munich.
Arsene Wenger amelaumu 'kiwango kibovu' baada ya kipigo cha Bayern Munich
Reviewed by Steve
on
Thursday, November 05, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment