Propellerads

Mourinho 'ammaindi' Schweinsteiger



Inasemekana kwamba kocha wa Manchester United, Jose Mourinho
amekasirishwa na mmoja wa viungo klabuni hapo.

Nyota wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger hivi karibuni alifunguka kwamba angependa kuendelea kukaa United pamoja na kwamba hayupo kwenye mipango ya Mourinho.

Kwa mujibu wa Daily Star , meneja huyo amekasirishwa na jinsi nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich alivyoamua kukaa klabuni.

Ripoti zinazidi kudai kwamba mchezaji huyo ametosa nafasi ya kuelekea klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon baada ya United kuelezwa kua wapo tayari kumlipa hata mishahara iliyosalia.

Jumanne hii, Mjerumani huyo aliweka wazi kwamba angependa kupambana ili kurejeshwa kwenye mipango ya Mourinho pamoja na kudaiwa kocha Mreno hana mpango wa kumweka kikosini.
Mourinho 'ammaindi' Schweinsteiger Mourinho 'ammaindi' Schweinsteiger Reviewed by Steve on Wednesday, August 31, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.