Mustafi aweka wazi aliyemshawishi kujiunga na Arsenal
Nyota mpya aliyesajiliwa na Arsenal amefichua aliyemshawishi kujiunga
na klabu hiyo ya London.
Mpango wa Gunners kumnasa Shkodran Mustafi kutoka Valencia ukiwa umekamilika, mchezaji huyo wa Ujerumani amefunguka kua ni Mjerumani mwenzake Mesut Ozil kujiunga na wakali hao.
"Sijaonana na Per (Mertesacker, kapteni wa Arsenal) kwa muda mrefu kwa sababu amestaafu mpira wa kimataifa, lakini nilizungumza na Mesut," Mustafi aliiambia Sky Sports Germany.
"Aliniambia kila kitu nilichotaka kufahamu. Kila kitu kilikua vizuri, kwa hiyo nilishawishika haraka. Haikuchukua muda sana.
"Siku zote niliipenda Arsenal, napenda jinsi wanavyocheza, sio kama waingereza.
"Mchezo hapa ni kama Hispania huku na timu ya taifa ya Ujerumani, kuweka mpira kwenye nyasi, kwa hiyo ilikua rahisi kunishawishi."
Mustafi aweka wazi aliyemshawishi kujiunga na Arsenal
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 31, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 31, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment