Propellerads

Cristiano Ronaldo aweka wazi umri atakaostaafu soka



Kapteni wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameweka wazi kua anataka kukaa kwa miaka mingine kumi ndani ya klabu yake ya Real Madrid, hivyo kutundika daruga akiwa na miaka 41.

Alhamisi hii Ronaldo alishinda tuzo ya mchezaji bora Ulaya ya UEFA ya 2016 baada ya kuisaidia Real Madrid kuchukua taji la Ulaya mara ya 11  huku pia akiiongoza Ureno kushinda taji la Euro mwaka 2016.

Ronaldo ameuita mwaka 2016 kama "usiosahaulika kwa klabu na nchi" na amekanusha madai kua anaingia hatua ya mwishoni katika wakati wake kwenye soka kwani anajiandaa kumalizia soka lake Santiago Bernabeu.

"Ulikua ni mwaka usiosahaulika kwa klabu na nchi, ilikua vizuri na nina furaha . [UEFA Best Player] ni taji muhimu sana, na baada ya kushinda makombe mawili makubwa zaidi kwa klabu na timu ya taifa, kushinda taji hili ni swala la kukumbuka sana huu mwaka." Ronaldo aliwaambia waandishi.

"Nipo katika klabu bora ulimwenguni na ninataka kustaafia hapa, nikifikisha 41, na kama nilivyosema kabla lengo langu ni kuongeza mkataba na kukaa."


Cristiano Ronaldo aweka wazi umri atakaostaafu soka Cristiano Ronaldo aweka wazi umri atakaostaafu soka Reviewed by Steve on Saturday, August 27, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.