Propellerads

Wenger ana uhakika asilimia 99 kuwasajili nyota hawa wawili



Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kua klabu yake ipo katika
hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa Shkodran Mustafi na Lucas Perez.

Klabu hiyo imekosolewa sana kwa kushindwa kufanya usajili wa maana majira haya, sasa wanaweza kutumia zaidi ya pauni mil 52 kukamilisha dili la wachezaji wawili.

Mustafi atawagharimu Arsenal kiasi cha pauni mil 35 ili kumtoa Valencia ambapo ni mipango ya Wenger kuimarisha safu yake ya Ulinzi baada ya  Per Mertesacker na Gabriel Paulista kuandamwa na majeraha.

Perez anatarajiwa kutua kwa wakali hao wa kaskazini mwa jiji la London kwa pauni mil 17 kuleta changamoto kwa Olivier Giroud upande wa mbele.

Alipoulizwa kuhusu wachezaji hawa wawili leo asubuhi kwenye mkutano na waandishi wa habari, Wenger aliwaambia waandishi "Tunashughulikia hizo dili. Tutasajili yeyote kabla ya dirisha halijafungwa, nina uhakika 99%."


Wenger ana uhakika asilimia 99 kuwasajili nyota hawa wawili Wenger ana uhakika asilimia 99 kuwasajili nyota hawa wawili Reviewed by Steve on Saturday, August 27, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.