Propellerads

Chelsea wapanga kumrejesha tena David Luiz kwa pesa ya kutosha tu



Imeripotiwa kwamba Chelsea wameweka ofa ya
pauni mil 32 kwa Paris Saint-German ili kumrejesha tena Stamford Bridge beki David Luiz.

Mbrazil huyo aliondoka Blues miaka miwili iliyopita kwa uhamisho ulioweka rekodi wa pauni mil 50 kuelekea PSG kuwasaidia kuimarisha ulinzi.

Hata hivyo Daily Mail wameripoti kua yupo tayari kurejea tena jijini London huku PSG wakiwa bado hawajaweka wazi endapo watamuuza beki huyo.

Inajulikana kwamba Chelsea wapo sokoni kwa ajili ya kutafuta beki wa kati kati baada ya kushindwa kumpata Kalidou Koulibaly kutoka Napoli na Alessio Romagnoli kutoka AC Milan msimu huu.


Chelsea wapanga kumrejesha tena David Luiz kwa pesa ya kutosha tu Chelsea wapanga kumrejesha tena David Luiz kwa pesa ya kutosha tu Reviewed by Steve on Wednesday, August 31, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.