Propellerads

Diego Costa aweka wazi alitaka kurejea Atletico Madrid



Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa amesisitiza kwamba ana furaha kuendelea
kubakia Stamford Bridge pamoja na kukubali kua alitaka kurejea Atletico Madrid msimu huu.

Baada ya kuwa na msimu wa pili usiopendeza akiwa na Blues, iliripotiwa kwamba nyota huyo angerejea klabu yake ya zamani kabla ya kuamua kuendelea darajani mwaka mwingine wa tatu.

Costa aliiambia AS "Kila mtu anajua kua kulikua na uwezekano wa kurejea Atletico lakini haikutokea kutokana na mambo kadhaa. Nawashukuru mashabiki na Cholo (Diego Simeone) kwa imani yake kwangu.

"Sasa nipo Chelsea, nina furaha na nimeanza nao msimu mpya. Ninaamini Atletico watafanya vizuri msimu huu kama mwaka jana na kushinda mataji. Nilitaka kurudi, siwezi kuongopa kuhusu hili."
Diego Costa aweka wazi alitaka kurejea Atletico Madrid Diego Costa aweka wazi alitaka kurejea Atletico Madrid Reviewed by Steve on Wednesday, August 31, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.