Propellerads

Yanaweza kutimia, Mourinho kubebeshwa virago!!


                       

Imeripotiwa kua Chelsea wanajiandaa kumtimua meneja Jose Mouriho kufuatia kupoteza mechi wakiwa nyumbani mbele ya Liverpool kwa 3-1 jana Jumamosi.

Mabingwa hao wa Premier League ambao walikua wamepoteza michezo mitano iliyopita kati ya kumi msimu huu kabla ya mtanange wa Liverpool, walijikuta wakiangukia pua tena huku ikiwa wazi matokeo mabovu yangeweza kugharimu kibarua cha kocha huyo Mreno.

Mourinho baada ya mechi aliwaambia waandishi kua alijiamini kwa kupewa nafasi ya kubadili mambo, lakini kwa mujibu wa The Mirror ,uongozi wa The Blues unafanya mipango ya kummwaga.

Maamuzi yanatarajiwa kufanywa kabla ya mechi ya klabu bingwa nyumbani dhidi ya Dynamo Kiev jumatano.

Akitimuliwa, Mourinho ambaye aliongeza mkataba mwezi Agosti anaweza kupewa kiasi cha pauni mil 9.5 kama fidia.

Chelsea bado wako nafasi ya 15 wakiwa nyuma kwa point 14 kwa vinara Ma City na Arsenal.
Yanaweza kutimia, Mourinho kubebeshwa virago!! Yanaweza kutimia, Mourinho kubebeshwa virago!! Reviewed by Steve on Sunday, November 01, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.