Van Gaal hana uhakika na nafasi ya Antony Martial

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amefunguka kua
bado hana uhakika kua Antony Martial anafaa zaidi kukaa nafasi gani.
Mfaransa huyo wa kimataifa alicheza upande wa kushoto dhidi ya Crystal Palace, lakini alishindwa kufunga ambapo Man United wamejikuta wakitoa sare ya 0-0.
Hata hivyo, Van Gaal amesisitiza kua nafasi yake, ambayo alikua anacheza nafasi ya kushoto mara kwa mara AS Monaco imemfanya kumpa shida katika kujua amweke nafasi gani.
"Bado hatujajua kwa sababu alicheza mara kwa mara AS Monaco kama winga wa kushoto," Van Gaal aliwaambia waandishi.
"Na mimi kama meneja natakiwa niangalie balance nzuri katika timu, na hiyo siyo rahisi sana. Kwa hiyo natakiwa kuamua kila wiki pia, inategemea na mipango ya mchezo na mpinzani na kadhalika.
"Tumemchezesha nafasi ya ushambuliaji, hiyo haikua mara yake ya kwanza, lakini Monaco mara nyingi alicheza wing ya kushoto mara kwa mara."
Martial alikua mchezaji kijana ghali zaidi aliposaini na Man United msimu huu.
Van Gaal hana uhakika na nafasi ya Antony Martial
Reviewed by Steve
on
Sunday, November 01, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, November 01, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment