Pamoja na kufungiwa, Mourinho atatumia mbinu hii kutoa maelekezo kwenye mechi na Stoke City

Jose Mourinho bado ataendelea kua na majukumu Chelsea ikipambana
na Stoke City Jumamosi hii pamoja na kufungiwa kuhudhuria mchezo huo.
Bosi huyo wa Chelsea alifungiwa kuhudhuria mechi moja uwanjani na kulipa faini ya pauni 40 000 kutokana na tabia aliyoionesha kwenye mechi dhidi ya West Ham ambapo walipoteza.
Pia jana Mourinho alikataliwa rufaa yake dhidi ya mashtaka mengine aliyonayo kutokana na tabia aliyoionesha kwenye mechi nyingine dhidi ya Southampton ambayo nayo pia walifungwa kwa 3-1.
Kocha huyo amesisitiza kua wachezaji watashuhudia kukosekana kwake uwanjani kesho, lakini bado wataweza kusikia maelekezo yake, hii ni kwa mujibu wa ripoti.
Mourinho anatarajiwa kuangalia mchezo akiwa katika hoteli ya timu na atawasiliana na jopo lake la ufundi kupitia simu ya mkononi. Ataweza kutoa maelekezo kwa timu yake, huku yeye akiwa kama , hayupo kwa sababu FA itawawia vigumu kufatilia mawasiliano hayo, hii ni kwa mujibu wa Daily Mail.
The Blues wako katika nafasi ya 15 msimamo wa ligi wakiwa wameshinda mara tatu kwenye mechi 11 ambapo Mourinho ana matumaini makubwa ya kupata point tatu muhimu japokua atakua akiangalia mechi akiwa hotelini.
Pamoja na kufungiwa, Mourinho atatumia mbinu hii kutoa maelekezo kwenye mechi na Stoke City
Reviewed by Steve
on
Friday, November 06, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, November 06, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment