Propellerads

Cristiano Ronaldo hashangazwi na hali ya Mourinho Chelsea


             


Cristiano Ronaldo amefunguka kua hashangazwi na kiwango cha
sasa cha Chelsea chini ya Jose Mourinho, lakini amesisitiza kua Mreno mwenzake anaweza kubadilisha mambo.

Mabingwa hao wa Premier League wako katika nafasi ya 15 baada ya kucheza mechi 11 na kushinda tatu pekee msimu huu huku ukiwa ni mwanzo mbaya zaidi tangu mwaka 1978.

Ronaldo ambaye amepata kucheza chini ya Mourinho kwa kipindi cha miaka mitatu alipokua akiifundisha Real Madrid, amesema kushuka huko hakumshangazi hata kidogo kutokana na mpira wa sasa jinsi ulivyo.

"Hali ya Mourinho!? Sishangai kwa sababu kwenye mpira chochote kinatokea," Nyota huyo wa Real Madrid aliiambia BBC Sport.

"Ni kweli, ni meneja niliyefanya nae kazi kwa miaka miwili na ninajua uwezo wake. Najua hii siyo yeye ila ni Chelsea wako katika wakati mgumu.

"Kama Mreno, ninataka kumuona Mourinho akiwa viwango vya juu siku zote. Kwa hiyo hicho ndicho ninachomtakia anaweza kutoka katika wakati mgumu alionao sasa na kuwafanya mashabiki wa Chelsea kua na furaha kwa sababu wanastahili hivyo."
Cristiano Ronaldo hashangazwi na hali ya Mourinho Chelsea Cristiano Ronaldo hashangazwi na hali ya Mourinho Chelsea Reviewed by Steve on Friday, November 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.