Propellerads

Kerr agoma Kessy asiuzwe, huenda Yanga ikawa sababu!!


         

Huku kandarasi ya beki wa Simba, Hassan Kessy ukielekea ukingoni
huku Yanga ikitajwa kuwa huenda ikamsajili beki huyo ikiwa tayari imeshaonyesha nia hiyo, Kocha Mkuu wa Simba, Dlyan Kerr amekuwa mkali kwelikweli baada ya kusikia taarifa hizo na kutamka: “He is not for sale”.

Kauli hiyo ya Kerr inamaanisha kuwa Kessy hawezi kuuzwa kwenda kokote, na kudai kuwa mipango aliyonayo kwa mchezaji huyo ni ya muda mrefu, hivyo ni vigumu kwake kukubali aondoke kirahisi.

“Kessy hatuwezi kumuuza kwa kuwa ni mmoja wa wachezaji wetu tegemeo, hawezi kwenda kokote hata Yanga ambapo nimesikia wanamtaka, nafikiri hizo ni tetesi na zitabaki kuwa tetesi,” alisema kocha huyo na kuongeza:

“Kama ni kuondoka basi ataondoka kwa dau kubwa sana, nimepanga kukutana na beki huyo na viongozi wangu kujua jinsi gani tunamshawishi Kessy ili aongeze mkataba mwingine kabla ya huu aliokuwa nao kumalizika.”


Inaelezwa kuwa kufikia mwezi ujao, Kessy ambaye alitua Simba akitokea Mtibwa Sugar, atakuwa amebakiwa na miezi sita ya mkataba wake, hivyo kwa mujibu wa kanuni za usajili, ataruhusiwa kuzungumza na klabu nyingine yoyote kuhusu suala la uhamisho.
Kerr agoma Kessy asiuzwe, huenda Yanga ikawa sababu!! Kerr agoma Kessy asiuzwe, huenda Yanga ikawa sababu!! Reviewed by Steve on Friday, November 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.