Propellerads

Haya ndio majibu ya Van Gaal kwa mashabiki wa Man United wanaozomea


             


Louis van Gaal amesema kelele za kuzomea za mashabiki wa
Manchester United zinatakiwa kuelekezwa kwake na sio kwa wachezaji.

Mashabiki walipiga kelele United washambulie kwenye mechi waliyoshinda kwa 1-0 dhidi ya CSKA Moscow jumanne iliyopita.

Walizomea tena kufuatia maamuzi ya Van Gaal kumtoa winga Antony Martial na kumuingiza Marouane Fellaini kabla Wayne Rooney hajafunga bao la ushindi dakika za mwishoni.

"Mashabiki wanatakiwa watoe ushirikiano vinginevyo wanafanya mambo kua magumu kwa wachezaji," alisema Van Gaal.

"Ni vigumu kuchezea Manchester United ukiwa na pressure kubwa na unaweza kuona hiyo Old Trafford kutokana na kelele.

"Kwa hiyo ni bora kumpigia kelele meneja, naweza kukabiliana na hilo kwa sababu nina uzoefu mkubwa na ni maisha yangu kama meneja."

Van Gaal amejikuta akikosolewa sana kutokana na mtindo wa uchezaji wa timu yake, huku mashabiki wengi wakidai magoli 15 kwenye mechi 11 haitoshi.

Hata hivyo United wako nafasi ya nne katika msimamo huku wakikabiliwa na mchezo dhidi ya West Brom hapo kesho.






Haya ndio majibu ya Van Gaal kwa mashabiki wa Man United wanaozomea Haya ndio majibu ya Van Gaal kwa mashabiki wa Man United wanaozomea Reviewed by Steve on Friday, November 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.