Neymar:Kwanini sipendi kuangalia mpira

Mshambuliaji wa FC Barcelona, Neymar amefichua kwanini hapendelei
mechi ambazo haziwahusishi wakali hao wa Catalan.
Mbrazil huyo aliyeifungia Barca kwenye mechi waliyoshinda 3-0 dhidi ya BATE Borisov katika Champions League jumatano, amefunguka kua hapendelei kuangalia timu nyingine zikicheza.
"Sipendi kutazama mechi kama Barcelona hawachezi," aliwaambia beIN Sports.
"Sitaki kuangalia mechi za Real Madrid. Sipendi kuangalia timu zingine. Siwezi kuhangaika kwa kitu nisichokiona."
Mchezaji huyo wa zamani wa Santos amecheza mechi 13 kwa Barca msimu huu, akifunga magoli 11 na kusaidia mengine saba.
Neymar:Kwanini sipendi kuangalia mpira
Reviewed by Steve
on
Friday, November 06, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, November 06, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment