'Ninajua nani wa kumlaumu kwa hali ya Chelsea, nimeona kwa macho yangu' Nyota wa zamani wa Chelsea afunguka

Mark Bosnich amesisitiza kua wachezaji wa Chelsea ndio wa
kulaumu kwa mwanzo wao mbaya msimu huu.
Mlinda mlango huyo wa zamani wa Manchester United ambaye pia aliichezea The Blues, anaamini ana nafasi ya kuangalia na kutoa mtazamo wake yeye kama mchezaji wa zamani wa klabu.
Meneja Jose Mourinho ametupiwa lawama nyingi huku kibarua chake kikiwa katika presha kubwa .
Huku baadhi ya ripoti zikidai wachezaji wanamgomea bosi wao, Bosnich anaamini ni rahisi sana kumnyooshea vidole kocha.
"Kwangu, mtazamo kama mchezaji wa zamani, daima wachezaji ni wa kuangalia kuliko meneja," aliiambia talkSPORT.
"Ndio, meneja anaweza kupanga mambo, lakini hawezi kwenda uwanjani na kucheza.
"Cha msingi ni kwamba haijalishi upande wako uko mzuri kiasi gani, kama ukiwa na wachezaji wanne au watano wanacheza chini ya kiwango , utapata shida.
"Hasa kwenye ligi kama Premier League, ambapo haieleweki ni timu gani inaweza kukufunga, ni mpambano kila wiki."
'Ninajua nani wa kumlaumu kwa hali ya Chelsea, nimeona kwa macho yangu' Nyota wa zamani wa Chelsea afunguka
Reviewed by Steve
on
Thursday, November 05, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, November 05, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment