Arsene Wenger :Pep Guardiola alitaka kujiunga Arsenal

Arsene Wenger amefichua kua bosi wa Bayern Munich,
Pep Guardiola alitaka kujiunga Arsenal kama mchezaji zaidi ya mwongo mmoja uliopita.
Guardiola, ambaye ataongoza kikosi chake kuwakaribisha Arsenal nyumbani kwenye klabu bingwa leo jumatano, aliwasiliana na Gunners kwa lengo la kucheza Londonhii ni kwa mujibu wa Wenger.
Badala ya kuhamia England, Guardiola alijiunga na klabu ya Brecia mwaka 2001 kisha kumalizia kipindi cha miaka 11 akiichezea Barcelona.
"Alitaka kucheza na mimi kama kocha wake," Wenger alinukuliwa akiiambia Sky Sport News "Alitaka kuchezea Arsenal. Nilikutana nae. Alikua na miaka 30 au 31.
"Siwezi kukumbuka vizuri, baada ya hapo alienda Italia na nilikua na wachezaji kama Patrick Vieira, Emmanuel Petit ambao walikua ni bado vijana huku pia wakichezea timu zao za taifa."
Wenger, ambaye alipata ushindi wa 2-0 nyumbani, anatarajia kua mgeni wa Bayern leo Allianz Arena kwenye mechi ya klabu bingwa.
Arsene Wenger :Pep Guardiola alitaka kujiunga Arsenal
Reviewed by Steve
on
Wednesday, November 04, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment