Van Gaal: Goli la Rooney sio muhimu sana

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal ametoa maoni
yake kuhusu goli la Wayne Rooney kwenye mechi ya jana ya klabu bingwa dhidi ya CSKA Moscow.
Rooney alitupia goli lake la kwanza kwenye michuano hii msimu huu na kuifikia rekodi ya Denis Law klabuni hao katika dakika ya 79, hivyo kumaliza ukame wa mabao Man United baada ya mechi nne mfululizo bila ushindi, lakini Van Gaal amesisitiza rekodi hiyo ya Rooney haimuhusu.
"Nilisema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba (Rooney) ni nahodha wangu.na anastahili sifa," Van Gaal aliiambia BT Sport "Lakini pia kwa sababu ni nahodha wangu ana sifa kubwa kwa sababu anafanya mambo mengi, kwa timu, kwa sababu ni kapteni. Hii ni muhimu sana.
"Bila shaka mshambuliaji anatakiwa afunge, lakini kwangu sio muhimu sana nani anafunga. Sasa hivi tuko juu ya hili kundi, tuna nguvu Premier League, tuko katika ratiba.
"Natumaini tutashinda dhidi ya West Bromwich lakini itakua kama hivi:tutashambulia na wao watalinda, na sio rahisi kuzivuruga timu za aina hii."
Mechi ya Premier League kati ya Man United na West Bromwich itakua Jumamosi hii.
Van Gaal: Goli la Rooney sio muhimu sana
Reviewed by Steve
on
Wednesday, November 04, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment