Cristiano Ronaldo: Mimi ni bora kuliko Messi

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kua katika
akili yake, yeye ni mchezaji bora kuliko Lionel Messi wa Barcelona.
Ronaldo na Messi ni wachezaji ambao wanatawala sana soka la sasa na pia wachezaji bora zaidi kila mmoja katika nafasi yake.
Mada ya nani mkali kati yao imekua ikiongolewa sana ndani ya kipindi cha miaka mitatu au minne iliyopita, lakini Ronaldo hana shaka kua nani ni bora zaidi kati yao.
"(kufananishwa na Messi) hakunisumbui. Ukiangalia miaka yangu nane iliyopita, siku zote nimekua juu. Nitajie mchezaji mwingine aliyefanya hivyo," aliiambia El Pais.
"Tofauti kati ya namba moja na namba mbili ni kitu kinachoeleza, kama ukishinda mataji au sivyo. Labda kwenu (waandishi), Messi ni bora, lakini akilini mwangu mimi ndiye."
Cristiano Ronaldo: Mimi ni bora kuliko Messi
Reviewed by Steve
on
Tuesday, November 03, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment