Propellerads

'Memphis Depay sio mchezaji wa timu'


                     

        

Bosi wa timu ya taifa ya Netherland, Danny Blind amemtaja mshambuliaji
wa Manchester United, Memphis Depay 'si mchezaji wa timu' baada ya kumwacha kwenye kikosi chake cha sasa.

Mchezaji huyo wa zamani wa PSV Eindhoven hayumo kwenye kikosi cha Blind kitakachopambana na Wales na Ujerumani kwenye mechi za kirafiki zitakazochezwa Novemba 11 na 17.

Kiwango cha Depay Man United kimemfanya asiwemo kwenye kikosi cha kwanza wiki za hivi karibuni Man United ambapo Blind hajamwita kwenye kikosi cha sasa pamoja na mfungaji wa muda wote wa mataifa Ulaya, Robin van Persie ambaye nae anaonekana kua katika wakati mgumu huko Uturuki msimu huu.

"Kwenye mpira unatakiwa ufanye kazi katika timu. Mara kwa mara hafanyi hivyo. Nadhani Depay ni mchezaji wa baadae, lakini kuna mambo mengine ya kuangalia. Pengine Louis van Gaal pia alisema kitu," Blind aliyeshindwa kuiwezesha Netherland kwa ajili ya Euro 2016, aliwaambia waandishi.

Depay aliyefunga mara tatu kati ya mechi 20 alizopata kucheza na timu yake ya taifa, hakuwemo kwenye mechi ya wikiendi Man United walipotoa sare ya 0-0 na Crystal Palace kutokana na majeraha.
'Memphis Depay sio mchezaji wa timu' 'Memphis Depay sio mchezaji wa timu' Reviewed by Steve on Tuesday, November 03, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.