Propellerads

Van Gaal ana furaha na ushindi dhidi ya CSKA Moscow


             

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kua
kikosi chake 'kimecheza vizuri' kwenye mechi yao ya klabu bingwa ambapo wameshinda kwa 1-0 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi nyumbani Old Trafford.

Iliwabidi Red Devils kungoja mpaka dakika ya 79 kupata goli, ambapo mshambuliaji Wayne Rooney alikomesha ukame wa muda wa dakika 404 kufunga magoli.

Baada ya kipenga cha mwiso, Van Gaal aliiambia BT Sport  kua alikua na furaha kuona timu yake ikipata ushindi tena baada ya mfululizo wa mechi tatu kwa sare pekee.

"Ni kama siamini kwa sababu tulitengeneza nafasi 12 ikabidi tusubiri kwa muda mrefu.

"Kabla ya hapo wangefunga na mechi ingekua tofauti. Kwa hiyo nina furaha. Tumecheza vizuri."


Van Gaal ana furaha na ushindi dhidi ya CSKA Moscow Van Gaal ana furaha na ushindi dhidi ya CSKA Moscow Reviewed by Steve on Wednesday, November 04, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.