Propellerads

Zlatan 'anashoboka' zaidi na nyota huyu wa Premier League




Zlatan Ibrahimovic amefichua ni mchezaji gani wa EPL anayemkubali
sana na anasikitika kwanini hajapata nafasi ya kucheza nae.

Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain amefunguka kumkubali nahodha wa Man United, Wayne Rooney katika documentary ya BBC iitwayo Wayne Rooney- The Man Behind The Goals.

"Kama siwezi kucheza nae, bado nitaendelea kumwangalia" alisema kama alivyonukuliwa na Daily Mirror.

"Hawa wachezaji wakubwa, wana wakati wao ndani ya mwaka mmoja hadi mitatu.

"Lakini kuendelea kwa miaka mitano ,kwa miaka 10 kama Wayne Rooney alivyofanya sio rahisi. Kuchezea timu kubwa kila siku ni pressure."

Ibrahimovic alienda mbali zaidi na kusema Wayne Rooney ndie alijituma zaidi huku Cristiano akiteka vichwa vya habari wakati walipocheza pamoja Man United.

"Alikimbia sana, alipambana sana, alijitoa sana." Mswedean aliongeza.

"Alipocheza na Cristiano Ronaldo, kazi yote ilifanywa na Wayne Rooney, lakini hakupata sifa kwa sababu Ronaldo alifunga magoli yote.

"Ningependelea zaidi awemo kwenye timu yangu kuliko kucheza dhidi yake. Bado sijawa na bahati ya kucheza nae, lakini nafurahia kumwona uwanjani."
Zlatan 'anashoboka' zaidi na nyota huyu wa Premier League Zlatan 'anashoboka'  zaidi na nyota huyu wa Premier League Reviewed by Steve on Thursday, October 01, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.